Trump kuwa mwenyeji wa viongozi watano wa Afrika
4 Julai 2025Trump atakutana na viongozi wa Gabon, Guinea-Bissau, Liberia, Mauritania na Senegal kwa majadiliano na chakula cha mchana siku ya Julai 9 katika Ikulu hiyo. Awali majarida ya Africa Intelligence na Semafor yalikuwa yameripoti kuwa serikali ya Trump itafanya mkutano wa kilele na nchi hizo tano za Kiafrika kutoka tarehe 9 hadi 11 Julai.
Afisa mmoja wa Ikulu ya White House amesema Trump anaamini kwamba nchi za Kiafrika zina fursa kubwa za biashara, ambazo zina manufaa kwa watu wa Marekani na washirika wao barani Afrika. Tangu aingie madarakani, Trump amechukuwa hatua kadhaa zinazoathiri mahusiano yake na mataifa ya Kiafrika, ikiwemo kupunguza misaada kwa kiwango kikubwa.
Mipango ya kustawisha nguvu ya kiuchumi ya Marekani
Utawala wa Trump umeondosha kwa kiwango kikubwa msaada kwa mataifa ya Afrika ikiwa kama sehemu ya mpango wa kubana matumizi inayozingatia, zingatio la kutimizwa kwa sera zisizoendana na hatua ya Trump ya kutoka kipaumbele kwa Wamarekani. Hatua hiyo inahimiza biashara na uwekezaji na pamoja na kutekeleza mipanga yenye kuzingatia ustawi wa pande zote.
Siku ya Jumanne, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alisema Marekani imeanza kuachana na kile alichokiita msaada wa kigeni unaotegemea hisani na mafasi itatolewa kwa yale mataifa ambayo yanaonyesha kwa pamoja uwezo na utayari wa kujisaidia.
Mapema mwezi Mei Afisa mkuu wa ofisi ya Masuala ya Afrika, Troy Fitrel alisema wajumbe wa Marekani barani Afrika watakadiriwa kwa zingatio la mipango ya kibiashara, akiielezea kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mkakati mpya wa msaada kwenye bara hilo.