Trump mwenyeji wa Ramaphosa ikulu ya White House Jumatano
21 Mei 2025Matangazo
Mkutano huo unaotazamiwa kuwa wenye mvutano na hisia kali, baada ya Trump kuituhumu Afrika Kusini kuruhusu "mauaji ya halaiki" yafanyike dhidi ya wakulima weupe walio wachache.
Afrika Kusini imeyakanusha vikali madai hayo na Rais Ramaphosa alishinikiza kufanyika kwa mkutano huo ili kuuokoa uhusiano wake na Marekani, ambao uko katika kiwango kibaya kuwahi kushuhudiwa tangu utawala wa ubaguzi wa rangi mwaka 1994.
Ramaphosa amesema katika mkutano huo, anatarajia kusahihisha kile alichokiita sifa mbaya za kuliharibia jina nchi yake.
Mkutano huo ndio utakaokuwa wa kwanza kati ya Trump na rais kutoka Afrika tangu arudi tena madarakani.