MigogoroUlaya
Trump kushirikiana na Erdogan kumaliza vita vya Ukraine
6 Mei 2025Matangazo
Trump ameeleza hayo kupitia ujumbe alouchapisha kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social mnamo usiku wa kuamkia leo, muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais Erdogan wa Uturuki.
Amesema anatarajia kushirikiana na Erdogan kuvimaliza haraka vita vya Ukraine alivyovitaja kuwa "havina msingi na venye athari kubwa". Trump pia amearifu kwamba Erdogan amemwalika kuitembelea Uturuki na vilevile kiongozi huyo wa Uturuki atakwenda Washington mnamo tarehe ambayo hakuitaja.
Uturuki iliyo mwanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO ina mahusiano mazuri na Urusi na Ukraine na mara kadhaa Rais Erdogan amesema nchi yake ni "sehemu mwafaka" ya kufanyika mazungumzo ya kumaliza vita vinavyoendelea.