Trump kupunguza uhusiano wa kidiplomasia na Afrika
29 Aprili 2025Rais wa Marekani Donald Trump sasa pia anakata uhusiano wa kidiplomasia wa serikali ya Marekani na bara la Afrika. Kulingana na mpango wa kubana matumizi wa Trump, karibu balozi 30 duniani kote zitafungwa zikiwemo nyingi barani Afrika.
Kulingana na rasimu ya amri ya rais ambayo maudhui yake yaliwekwa wazi na gazeti la Marekani The New York Times, "upangaji upya kamili wa kimuundo" wa wizara ya mambo ya nje umepangwa kufikia Oktoba 1.
Lakini Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alijibu mara moja kupitia chapisho kwenye mtandao wa X, akiita "habari za uwongo".
Uteuzi wa mabalozi sio kipaombele kwa Trump
Kufikia sasa, utawala wa Trump umeteua mabalozi watatu katika bara la Afrika: kwa Afrika Kusini, Morocco, na Tunisia. "Uteuzi wa mabalozi sio kipaumbele kwa utawala wa Trump, na pia katika nchi nyingine zote, tayari kuna mabalozi ambao bado wanahudumu au nafasi zilizo wazi," Alex Vines, mkuu wa mpango wa Afrika katika taasisi ya wataalam yenye makao yake makuu London, Chatham House, aliiambia DW.
Utawala wa Trump wafuta zaidi ya 80% ya miradi ya USAID
Orodha ya sasa ya Jumuiya ya Huduma za Kigeni ya Marekani - chama cha kitaaluma cha huduma ya kigeni ya Marekani, inaonyesha kuwa kwa sasa hakuna kujumuishwa kwa mataifa madogo, lakini pia kuhusu suala la ni nani ataiwasilisha diplomasia ya serikali ya Marekani kwa mataifa yaliyoimarika kiuchumi kama vile Nigeria, Kenya, Misri na Ethiopia, katika siku zijazo.
Lesotho, Eritrea, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kongo , Gambia , na Sudan Kusini ziko kwenye orodha ya balozi zitakazofungwa, pamoja na balozi ndogo huko Douala, Cameroon, na Durban, Afrika Kusini.
Balozi wa Afrika Kusini asema hajutii kurudi kwake nyumbani
Rais Trump wa Marekani hivi majuzi alimteua Leo Brent Bozell III kama balozi mteule, akisubiri kuthibitishwa na baraza la seneti la Marekani.
Uteuzi wa Bozell unafuatia hatua ya Marekani ya kumuondoa balozi wa Afrika KusiniEbrahim Rasoolkutokana na maoni yake ya kumkosoa Trump, ambayo yalisababisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili katika hali mbaya.
"Bozell ni mkosoaji mkuu wa vyombo vya habari vya kihafidhina na huenda akawa uteuzi mgumu kwa Afrika Kusini," amesema Steven Gruzd, mkuu wa Mradi wa Afrika na Urusi katika Taasisi ya Masuala ya Kimataifa ya Afrika Kusini.
Trump alisimamisha misaada ya kifedha kwa nchi hiyo, hatua ambayo pia inaathiri miradi ya misaada katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI, na ina madhara makubwa kwa watu.
Ramaphosa: Kuimarisha uhusiano na US ni kipaumbele chetu
Tangu aingie madarakani mwezi Januari, Trump amechukua hatua kali za kusitisha ufadhili na kufunga afisi za umma, huku serikali ikiendeshwa na Idara ya Ufanisi wa Serikali (DOGE) inayoongozwa na Elon Musk, mshauri mkuu wa Rais Trump, idara ambayo inafuatilia juhudi kubwa za kuipunguzia serikali shinikizo. Aidha, Wizara ya Mambo ya Nje itapunguzwa kama sehemu ya mageuzi ya kimkakati.