Trump kumkaribisha Starmer White House
27 Februari 2025Matangazo
Starmer atakuwa kiongozi wa pili wa Ulaya kukutana na Trump ndani wiki hii baada ya Rais Emmanuel Macron kumtembelea Trump siku ya Jumanne. Macron aliyaweka mezani mashaka ya Ulaya juu ya mpango wa amani ya Ukraine ulianzishwa na Trump.
Waziri Mkuu Starmer anatumai ataweza kumshawishi Trump kuwa amani ya kudumu nchini Ukraine itapatikana pale serikali mjini Kyiv na viongozi wa Ulaya watakapokuwa sehemu ya mazungumzo na Urusi.
Viongozi wa bara hilo wana wasiwasi kuwa shinikizo la Trump la kuyaharakisha mazungumzo hayo litatoa mwaya wa kuilazimisha Ukraine ikubali kupita kiasi matakwa ya Rais Vladimir Putin wa Urusi.