Trump kukutana na Mfalme Abdullah
11 Februari 2025Matangazo
Pendekezo hilo la Trump limezusha ukosoaji kutoka mataifa karibu yote ya kiarabu ikiwemo Jordan, ambayo yanapinga mipango yoyote ya kuwaondoa Wapalestina kutoka kwenye ardhi inayozingatiwa kuwa sehemu ya taifa ya lao pindi litakapoundwa.Trump tayari ameashiria kuwa tayari kusitisha misaada kwa Jordan na Misri iwapo zitakataa mpango wake wa kuwahamisha Wapalestina. Kwenye mazungumzo ya leo, Mfalme Abdullah anatarajiwa kumtanabahisha Trump kwamba hatua zozote za kuipoka ardhi ya Gaza zitasababisha kushamiri wa makundi ya itikadi kali, machafuko kwenye kanda ya mashariki ya kati na kuiweka rehani amani ya Israel.