Trump atishia kuiwekea Canada ushuru mkubwa
31 Julai 2025Matangazo
Trump ameitishia Canada akisema itakuwa vigumu mno kufikia makubaliano hasa baada ya Canada kutangaza kuwa inapanga kulitambua Taifa la Palestina katika hadhara Kuu ya Umoja Mataifa mwezi Septemba.
Trump anatazamiwa kuziwekea ushuru wa asilimia 35, bidhaa zote za Canada ambazo hazihusiki na makubaliano ya biashara ya pande tatu kati ya Marekani- Mexico na Canada. Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney amesema mazungumzo na Washington yalikuwa chanya lakini hayawezi kukamilika kabla ya tarehe ya mwisho ya Agosti 1.