MigogoroUlaya
Trump awatolea wito Putin na Zelensky kufikia makubaliano
28 Aprili 2025Matangazo
Aidha Trump ameusifu mkutano wao siku ya Jumamosi mjini Vatican, huku akimtaka pia rais wa Urusi Vladimir Putin kusitisha mashambulizi nchini Ukraine na kukaa kwenye meza ya majadiliano ili kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano.
Soma pia: Trump achukua hatua ya nadra ya kumkosoa Putin kuhusu vita vya Ukraine
Kauli za Trump zimetolewa wakati Moscow na Kiev zikiendelea kushambuliana vikali kwa makombora na droni, huku Korea Kaskazini ikithibitisha kuwa imewatuma wanajeshi wake nchini Urusi kusaidia katika vita hivyo hasa katika ukombozi wa eneo la mpakani la Kursk.