Trump ausuta Umoja wa Ulaya katika mkutano wa Davos
27 Januari 2025Katika hotuba ya takribani saa moja kwa viongozi wa kibiashara na kisiasa waliokusanyika katika Kongamano la Kiuchumi la Dunia huko Davos, Uswisi, Trump alisema Marekani inatendewa "yasiyo ya haki" na "mabaya sana" na Umoja wa Ulaya kutokana na sheria zake za biashara na biashara kwa jumla.
Trump alisema hatavumilia nakisi ya biashara ya Marekani na Umoja wa Ulaya na pia aliushutumu umoja huo kwa kukataa kununua bidhaa za kilimo na magari kutoka Marekani.
Trump ahutubia Kongamano la Uchumi la Dunia mjini Davos
"Kwa mtazamo wa Amerika, Umoja wa Ulaya unatutendea vibaya sana. Wana kodi kubwa ambayo tunajua kuhusu na kodi ya VAT, na ni kubwa sana. Hawachukui bidhaa zetu, kimsingi, hawachukui bidhaa zetu za shambani na hawachukui magari yetu, ilhali wanatutumia magari kwa mamilioni. Wanaweka ushuru kwa vitu ambavyo tunataka kufanya," alisema Trump.
Wakati wa kampeni zake za uchaguzi, Trump alitaja mipango ya kuanzisha kutoza ushuru mpya wa 10% hadi 20% kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Umoja wa Ulaya.