Trump atishia kuiwekea Urusi vikwazo isipoafiki amani
27 Agosti 2025Matangazo
Trump amekuwa akishinikiza mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Putin na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky lakini akisisitiza kuwa Zelensky si mtakatifu pia katika mzozo huo.
Trump asema atakutana 'haraka sana' na Putin.
Ukraine na mataifa ya Ulaya yamekuwa na wasiwasi kwamba juhudi za upatanishi za Trump zinaweza kumalizikia kwa kuitaka Kiev kusalimisha baadhi ya maeneo yake kwa Urusi kwa maslahi ya kupata makubaliano ya amani.