Trump athibitisha mkataba wa amani kati ya Kongo na Rwanda
21 Juni 2025Akithibitisha kuhusu makubaliano hayo yaliyofikiwa na mataifa hayo mawili ya Afrika Mashariki na ambayo yanatarajiwa kusaini rasmi mkataba wa amani wiki ijayo mjini Washington, Trump kupitia chapisho lake kwenye mtandao wa Truth Social, amesema ilikuwa ni siku njema kwa Afrika na kwa dunia nzima.
Trump na Ramaphosa waibua matumaini mapya ya amani kati ya Rwanda na DRC
Trump ameongeza kuwa amekuwa akipuuzwa na Kamati ya Nobel ya Norway kwa jukumu lake la upatanishi katika migogoro mbalimbali ikiwa ni pamoja na ule wa India na Pakistan, pamoja na Serbia na Kosovo.
Pia, alitaka kutambuliwa kwa juhudi zake za kudumishaamani kati ya Misri na Ethiopia na kusimamia Mkataba wa Abraham, uliopelekea msururu wa makubaliano yaliyolenga kurejesha uhusiano kati ya Israel na mataifa kadhaa ya Kiarabu.