Marekani na Uingereza zatangaza mkataba muhimu wa kibiashara
9 Mei 2025Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer anasema mpango huo unalinda kampuni za kutengeza magari za Uingereza na watengenezaji wa chuma. Tangu ilipoondoka kwenye Umoja wa Ulaya mnamo 2020, Uingereza imedhamiria kupanua uhusiano wa kibiashara wa kimataifa nje ya umoja huo.
Lakini wakati Umoja wa Ulaya uliathiriwa na ushuru wa 20% uliotangazwa na Rais Trump, ushuru uliowekwa dhidi ya Uingereza ulikuwa 10% tu. Lakini makubaliano ya kibiashara na Marekani yanaonekana kuwa muhimu kwa serikali ya Starmer. Uingereza mapema wiki hii ilifikia makubaliano ya biashara huria na India - mkataba mkubwa zaidi wa kibiashara tangu mchakato wa Brexit.
Wakati huo huo, maafisa kutoka Marekani na China watakutana Uswisi Jumamosi kutafuta suluhu ya vita vya kibiashara kati ya mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa duniani.