Trump asitisha msaada wa kijeshi kwa Ukraine
4 Machi 2025Trump mapema Jumatatu alikuwa amekataa kufuta uwezekano wa kusitisha msaada huo wakati alipoulizwa na waandishi, lakini usitishwaji wowote wa silaha za Marekani kwenye uwanja wa mapambano utadhoofisha pakubwa nafasi ya Ukraine kuukabili uvamizi wa Urusi. Afisa mmoja wa Ikulu ya White House amesema Trump amekuwa wazi kuwa lengo lake ni amani. Trump na Zelensky walilumbana hadharani katika Ikulu ya White House Ijumaa wiki iliyopita.
Na anahitaji washirika wake kujitolea katika lengo hilo pia. Amesema wanasitisha kwa muda na kutathmini msaada wake kwa Ukraine ili kuhakikisha kuwa unachangia katika kupata suluhisho.
Gazeti la New York Times limeripoti kuwa kusitishwa huko kumeanza kutekelezwa mara moja na kutaathiri silaza zenye thamani ya mamia ya mamilioni ya dola zilizopaswa kupelekwa Ukraine. Zelensky alisema Jumatatu kuwa anataka vita hivyo vimalizike haraka iwezekanavyo.