Trump asema wanazungumza na Putin kumaliza vita Ukraine
1 Februari 2025Matangazo
Rais Donald Trump ametangaza Ijumaa kuwa utawala wake tayari umefanya mazungumzo "makubwa" na Urusi kuhusu vita vya Ukraine, na kwamba yeye na Rais Vladimir Putin wanaweza kuchukua hatua "muhimu" hivi karibuni kumaliza mzozo huo.
Hata hivyo, Trump hakusema ni nani kutoka utawala wake aliyezungumza na Warusi, lakini alisisitiza kuwa pande hizo mbili "zinaendelea kuzungumza."
Tangu alipochukua madaraka tena, Trump amemkosoa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy, akisema kuwa alipaswa kufikia makubaliano na Putin ili kuepusha vita.
Wakati huo huo shambulio la kombora la Uirusi katikati mwa mji wa Ukraine wa Odesa, Ijumaa usiku, limewajeruhi watu saba na kuharibu majengo ya kihistoria.