Trump amwalika Netanyahu Ikulu ya White House
29 Januari 2025Matangazo
Tangazo hilo linatolewa wakati Marekani ikiendelea kuzishinikiza Israel na Hamas kuendeleza makubaliano ya kusitisha mapigano, yaliyosimamisha vita vya miezi 15 kwenye Ukanda wa Gaza.
Sehemu ya barua ya Ikulu ya White House iliyosambazwa na ofisi ya Netanyahu imemnukuu Trump akisema anataraji kujadiliana na Netanyahu juu ya namna ya kuleta amani kwa taifa la Israel na majirani zake pamoja na juhudi za wapinzani wao wa pamoja.
Mkutano wa Februari 4 ni fursa kwa Netanyahu, anayekabiliwa na shinikizo nyumbani, kuukumbusha ulimwengu kuhusu uungwaji mkono wa muda mrefu wa Trump, pamoja na namna anavyotetea vita vya Israel dhidi ya Hamas.