Trump amtuma tena Witkoff kwenda Moscow
4 Agosti 2025Matangazo
Akizungumza jioni ya Jumapili (Agosti 3), Trump aliwaambia waandishi wa habari kwamba Warusi ni wazuri kwenye kukwepa vikwazo na kwamba alikuwa anamtuma Steve Witkoff kwenda kuangalia kinachoweza kufanyika.
Witkoff alitazamiwa kuwasili Moscow ama Jumatano au Alhamis, siku za mwishoni kabisa kabla ya muda wa mwisho uliowekwa na Trump kumalizika.
Trump alitishia kuiwekea vikwazo vikali zaidi Urusi endapo haikutekeleza matakwa yake hayo.
Hayo yanakuja wakati Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine akisema wamekubaliana na Urusi kubadilishana wafungwa 1,200 wa kivita kufuatia majadiliano yao yaliyofanyika nchini Uturuki mwezi uliopita.
Urusi haijasema chochote kuhusu ziara ya Witkoff wala mabadilishano ya wafungwa.