Trump amtuhumu Ramaphosa kwa mauaji wa wazungu
22 Mei 2025Rais wa Marekani Donald Trump, alimshambulia kwa maneno rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini,akimtuhumu kwamba serikali yake imekuwa ikiendesha mauaji ya kimbari dhidi ya waafrika Kusini wazungu na kutwaa kwa nguvu ardhi ya wakulima wakizungu.
Katika mkutano baina ya viongozi hao uliofanyika ikulu mjini Washington,Trump alicheza mkanda wa video aliodai unathibitisha mauaji ya kimbari yaliyotokea dhidi ya wazungu nchini Afrika Kusini, huku akisema mwanasiasa wa upinzani nchini Afrika Kusini Julius Malema anapaswa kukamatwa.
Ramaphosa alikanusha tuhuma za kufanyika mauaji ya kimbari katika nchi yake ambayo imepitia historia ya maumivu makali yaliyosababishwa na utawala wa ubaguzi wa rangi ulioongozwa na wazungu.
Ziara ya Ramaphosa Washington ilikuwa na lengo la kurekebisha mahusiano kati ya nchi yake na Marekani.