Trump amfukuza kazi mkuu wa idara ya takwimu za ajira
2 Agosti 2025Matangazo
Rais Trump bila ya kutoa Ushahidi wowote amemshutumu Bi. Erika McEntarfer, kwa kuchakachua data za ajira kwa sababu za kisiasa ambazo amesema zinalenga kukichafua chama cha Republican na yeye kama Rais wa Marekani aonekane mbaya, baada ya ripoti mpya kuonyesha nyufa katika soko la ajira la Marekani.
Rais Trump amesema nafasi ya mkuu huyo wa idara inayoshughulikia takwimu za ajira itachukuliwa na mtu mwengine mwenye uwezo mkubwa zaidi.
Ripoti iliyochapishwa na idara hiyo ya takwimu za ajira imebainisha nafasi za ajira zilizoongezeka mwezi uliopita zilikuwa ndogo.