Trump amaliza ziara mataifa matatu ya Ghuba
16 Mei 2025Matangazo
Mwenyewe amesema ziara hiyo imeimarisha "nafasi ya Washington kwenye kanda hiyo na ulimwenguni"
Mapema leo asubuhi Trump na mwenyeji wake Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan walikuwa na mkutano na viongozi wa makampuni makubwa ya biashara kutoka sekta za afya, usafiri wa anga na nishati.
Trump anaondoka kwenye kanda hiyo akiwa ametiliana saini mikataba ya kibiashara yenye thamani ya karibu dola Trilioni 4 ikiwemo uwekezaji wa dola Trilion 1.4 uliotangazwa na Umoja wa Falme za Kiarabu jana Alhamisi.
Mapema wiki hii Trump aliitembelea Saudi Arabia na baadaye Qatar katika ziara iliyotuama juu ya masuala ya uwekezaji na hali ya usalama kwenye kanda ya Mashariki ya Kati.