Rais wa Marekani Donald Trump ameapa kuendeleza juhudi zake za kubadili uchumi, uhamiaji na sera za kigeni katika hotuba yake bungeni ikiwa ni wiki sita baada ya kuanza kwa muhula wake wa uongozi. Trump ameliambia bunge la nchi hiyo kuwa anafanya juhudi za kuvimaliza vita vya Urusi na Ukraine, na kwamba baadae wiki hii, atatangaza upanuzi wa uzalishaji wa madini muhimu nchini humo.