Trump aiweka polisi ya Washington chini ya serikali kuu
12 Agosti 2025Jeshi limesema kati ya idadi hiyo kubwa ya askari wa ulinzi watakaoplekewa mjini humo ni askari 100 hadi 200 watakaoonekana barabarani.
Uamuzi wa Trump wa kumuelekeza Waziri wa Ulinzi Pete Hegseth kupeleka askari hao wa ulinzi Washington, ni mfano mwengine wa Trump kutuma askari hao kuunga mkono kufurushwa kwa wahamiaji au kupambana na makundi ya wakaazi na maafisa wa usalama wanaopinga hatua kali zinazochukuliwa dhidi ya wahamiaji.
Trump aiweka polisi ya Washington chini ya serikali kuu
Rais Trump ameiweka idara ya polisi ya jiji la Washington chini ya udhibiti wa serikali kuu, akitaja kile alichokiita mji uliotawaliwa na "magenge ya ukatili na wahalifu wanaosababisha umwagaji damu."
Uamuzi wa Trump ulikumbwa na ukosoaji mkali kutoka kwa Meya wa D.C. Muriel Bowser, ambaye aliuita "unaotatiza” na akatoa takwimu zinazoonesha kuwa uhalifu wa kutumia nguvu katika mji huo mkuu ulipungua kwa asilimia 35 mnamo 2024 na asilimia 26 zaidi katika nusu ya kwanza ya 2025.