Rais wa Marekani Donald Trump ameliweka Jeshi la Polisi la Washington, D.C. chini ya udhibiti wa serikali kuu, akidai kuna dharura ya uhalifu, licha ya takwimu kuonyesha kiwango cha uhalifu kupungua kwa kasi miaka 2 iliyopita. Kuitazama kwa kina hatua hii Tatu Karema alizungumza na mwandishi wa Marekani, Mubelwa Bandio akiwa Maryland na akamuuliza kuhusu uwezekano wa kufanikiwa kwa azma ya Trump.