Trump aitaka Qatar kuishawishi Iran mpango wake wa nyuklia
15 Mei 2025Trump ametoa wito huo wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa ajili yake na Emir wa Qatar Sheikh tamim bin Hamad Al Thani.
Awali katika mkutano Baraza la Ushirikiano la Ghuba, rais huyo wa Marekani alisema anataka makubaliano na Iran, ila jamhuri hiyo ya kiislamu ni lazima iache kuyaunga mkono makundi ya kiwakala ya wanamgambo Mashariki ya Kati.
Iran ilifikia makubaliano na utawala wa Barack Obama mwaka 2015 ikikubali kurutibisha madini ya urani kwa hadi asilimia 3.67, ila makubaliano hayo yalifutwa katika utawala wa kwanza wa Trump.
Haya yanajiri wakati ambapo Trump ameingia mikataba ya kibiashara na Qatar katika ziara yake hiyo ya eneo la Ghuba.
Kulingana na ikulu ya White House, kampuni ya utengenezaji ndege ya Marekani ya Boeing imepata mkataba wa kulitengenezea shirika la ndege la Qatar, ndege 160 zenye thamani ya dola bilioni 96.