Trump afikiria kupunguza balozi za Marekani barani Afrika
21 Aprili 2025Kulingana na rasimu ya amri ya rais Trump ambayo bado haijatangazwa, ni kwamba mageuzi kamili ya kimuundo ya Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani yataanza kutekelezwa ifikapo Oktoba 1 mwaka huu.
Mabadiliko makubwa zaidi yatakuwa kupanga juhudi za kidiplomasia za Marekani katika kanda nne : Ulaya na Asia, Mashariki ya Kati, Amerika ya Kusini na Asia-Pasifiki.
Kwa mujibu wa rasimu hiyo ya amri ya rais ni kwamba ofisi ya sasa ya masuala ya Afrika kwenye wizara ya mambo ya nje itafutwa, na kurudiliwa na Ofisi ya Mjumbe maalum wa Masuala ya Afrika ambaye atakuwa akitoa ripoti katika Ikulu ya White House, badala ya Wizara ya Mambo ya Nje.
Pia, rasimu ya amri hiyo inasema balozi zote zisizo muhimu barani Afrika, katika eneo la kusini mwa Jangwa la Sahara, zitafungwa.