Trump amkosoa Putin kuhusu vita vya Ukraine
24 Aprili 2025Katika ujumbe aliouandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, Trump amesema hafurahishwi na mashambulizi hayo ya Urusi ambayo ameyaitwa yasiyostahili na yaliyofanywa kwa wakati mbaya.
Ameendelea kusema kuwa wanajeshi elfu tano wanafariki dunia kila wiki katika vita hivyo na kumtaka Putin wakubaliane kuhusu mkataba wa amani.
Hatua hii ya Trump kumkosoa Putin ambaye ndiye aliyeanzisha vita hivyo, ni ya nadra kwa kuwa mara kadhaa amesema Urusi ina nia ya kufikia makubaliano ya amani kuliko Ukraine.
Hayo yanafanyika wakati ambapo chanzo cha kijeshi cha Urusi kimeliambia shirika la habari la Reuters kuwa, silaha iliyowauwa angalau watu 8 katika shambulizi la Urusi lililofanywa usiku wa kuamkia leo huko Kyiv, lilikuwa kombora la Korea Kaskazini.