Trump aanza ziara mataifa matatu ya kiarabu
13 Mei 2025Matangazo
Trump alilakiwa na Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia kwenye uwanja wa ndege mjini Riyadh na mchana huu atashiriki karamu aloandaliwa na mwenyeji wake kwenye kasri la nchi hiyo.
Miongoni mwa ajenda muhimu za ziara yake ni pamoja na njia za kuuumaliza mzozo wa Gaza, kupunguza bei ya nishati ya mafuta na juhudi za Marekani za kuishinikiza Iran kuachana na mradi wake wa nyuklia.
Trump anatumai uamuzi wake wa kuzitembelea nchi hizo tatu katika ziara yake ya kwanza rasmi nje ya nchi tangu aliporejea madarakani, atamudu kuimarisha ushawishi wa Marekani kwenye eneo la Ghuba na kanda nzima ya Mashariki ya Kati.