Trump aandaa dhifa ya chakula kwa viongozi wa Afrika
9 Julai 2025Matangazo
Kwa mujibu wa ofisi ya rais wa Liberia, viongozi hao wanajadili ushirikiano katika maendeleo ya kiuchumi, usalama, miundombinu na demokrasia.
Rais Joseph Boakai wa Liberia amesema anatarajia matokeo chanya na amesisitiza dhamira ya nchi yake kwa utulivu na ukuaji wa kiuchumi wa kikanda.
Trump kupunguza uhusiano wa kidiplomasia na Afrika
White House haikutoa taarifa zaidi kuhusu mkutano huo ambao umefanyika ghafla, huku utawala waTrumpukiendeleza juhudi za kujipanga upya katika sera zake kuelekea bara la Afrika.