Trump aagiza kuwekwa nyambizi za nyuklia baada ya malumbano
2 Agosti 2025Matangazo
Hata hivyo Trump hakutoa maelezo zaidi licha ya kuhalalisha uamuzi wake kwa kile alichokieleza kuwa "kauli za uchochezi mkubwa" za rais wa zamani wa Urusi Dmitry Medvedev.
Hivi karibuni Medvedev aliyakosoa vikali matamshi ya mara kwa mara ya Trump kuhusiana na vita vya Ukraine. Rais huyo wa zamani ambaye kwa sasa ni makamu mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Kitaifa anazingatiwa kuwa mtu wa karibu wa Rais wa Urusi Vladimir Putin.