UchumiAmerika ya Kaskazini
Trump aanza mazungumzo na Waziri Mkuu wa India Modi
14 Februari 2025Matangazo
Rais Trump amesema wataanzisha mazungumzo ya kushughulikia mivutano ya muda mrefu ambayo ingeweza kushugulikiwa zaidi ya miaka minne iliyopita. Trump alisema
"Tutaimarisha uhusiano wetu wa kiuchumi na kuleta usawa zaidi katika uhusiano wetu wa kibiashara."
Aidha aliongeza kwamba hatua hiyo ni shara ya nia njema, kutokana na Waziri Mkuu wa India Modi kutangaza kupunguzwa kwa ushuru usio wa haki, na mkubwa wa India unaoizuia kabisa Marekani kulifikia soko la India.
Soma pia:Trump na Modi waafikiana suala la urari wa biashara
Modi kwa upande wake amesema makubaliano baina ya mataifa hayo yatakamilishwa hivi karibuni na ananuia kuongeza biashara kwa hadi dola bilioni 500 ifikapo mwaka 2030, huku ajenda ya nishati ikitiliwa kipaumbele.